Ubadhirifu TFF

bri wanaJF,
Ufisadi TFF, zaidi ya bil 1.1 zachotwa
ndani ya wiki moja, Nani anamlinda
Malinzi nyuma ya pazia? na PCCB
wanaogopa kumpandisha kizimbani
Bwana Malinzi kwasababu gani ikiwa
uchunguzi wameshakamilisha?
Ndugu zangu wanaJF, Maafisa wa Tume
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
PCCB makao makuu wamekamailisha
uchunguzi dhidi ya pesa zilizochotwa
katika akaunti ya TFF ndani ya wiki moja
zaidi ya TZS bil 1 za kitanzania mwezi
Agosti 2016.
Aidha PCCB ilishawahoji Jamal Malinzi
rais wa TFF, Mwesigwa Selestine katibu
mkuu wa TFF zaidi ya mara nne kutaka
maelezo juu ya pesa hizo zilitolewa katika
akaunti ya shirikisho na kwenda
kusikojulikana. Inasemekana fedha hizo
zimetumika kwenye kampeni za chaguzi
za mikoa kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF
mwaka huu 2017.
Naomba ifahamike kuwa Shirikisho la
mpira wa miguu(TFF) walipokea fedha
hizo kutoka FIFA kwa ajili ya maendeleo
ya mpira wa miguu nchini hususani vijana
na wanawae, lakini katika hali ya
kushangaza zimechukuliwa kwa matumizi
binfasi ya wakuu wa taasisi hiyo bila
kufuata taratibu za kikatiba
zinazoliongoza shirikisho hilo.
Inasemekana kati ya Julai – Agosti pesa
zaidi ya bil 1.2 zilichotwa katika akaunti
ya TFF, baada ya Malinzi na Mwesigwa
kufoji muhtasari na sahihi za wajumbe wa
Utendaji kwenda benki ukionyesha kuwa
wametoa baraka ya kubadilisha
anayesaini hundi za malipo(signatory) za
taasisi hiyo.
Hata hivyo kabla ya kuchota pesa hizo
Bwana Malinzi alimuagiza ndugu
Mwesigwa kumuandikia barua ya kwenda
likizo kwa lazima aliyekua mkurugenzi wa
fedha TFF, Edgar Masoud kisha kumuajiri
binti anayeitwa Nsia na kumkabidhi
nafasi ya kusaini hundi za malipo,
ambapo ndani ya wiki moja waliweza
kuchota dola za kimarekani 425,000 (sawa
na mil 910,000,000 za kitanzania) bila
ridhaa ya kamati ya utendaji.
Hata Edgar aliporejea ofisi baadaya likizo
yake kumalizika katikati ya mwezi Agosti,
alipewa barua ya kuachishwa kazi ndani
ya mwezi huo huo, Edgar alifungua kesi
ya madai dhidi ya TFF kuvunja mkataba
wake inayotarajiwa kutolewa hukumu
mwezi Februari mwishoni.
Aidha Malinzi alitoa maelekezo ya kulipwa
kiasi cha milioni 70 za kitanzania swahiba
wake kwa Michael Wambura, ambaye
deni lake dhidi ya TFF lilishafutwa tangu
enzi za utawala wa Leodgar Tenga, baada
ya kamati ya utendaji wakati huo kukataa
madai hayo na kufikiwa muafaka wa
kutolipwa.
PCCB imeshakamilisha kuwahoji wajumbe
wote wa kamati ya Utendaji wanaoishi
Dar es salaam ambao ni Ayoub Nyenzi,
Wilfred Kidao, Georfey Nyange ‘Kaburu’,
Ahmed Mgoyi, Ramdhan Nassib na
makamu wa Rais TFF Wallace Karia
waliotoa ushahidi dhidi ya malipo hayo
kufanyika pasipo idhini ya kikao ya
Kamati ya Utendaji.
Katika sakata hilin wengine walioitwa
kutoa ushahidi kutoka Sekretatiat ya TFF
ni Daniel Msangi (Kaimu Mkurugenzi wa
Fedha), Jonas Kiwia (Mkurugenzi wa
mashindano), Salum Madadi (Mkurugenzi
wa Ufundi), Hellen Adam (Mlipaji),
Boniface Wambura (Afisa Mtendaji wa
Bodi ya Ligi).
Katika hali ya kushangaza, Malinzi
amekua akilia kwa waziri mkuu Kassim
Majaliwa, Waziri wa Habari, Utamaduni
na Michezo Nape Nnauye kupitia msaidizi
wake Juma Matandika (anayetoka sehemu
moja na waziri mkuu – Ruangwa, lakini
pia ndio mwenye kesi na PCCB ya
kuomba rushwa Geita Gold mil 25 ili timu
yao ipande daraja) kuwa watu wa mpira
wanamuonea wivu, kitu kinachoonyesha
kama PCCB kushikwa na kigagaziko
kuwapandisha kizimbani Malinzi pamoja
na Mwesigwa.
> Malinzi na Mwesigwa wanatakiwa
kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya
ofisi, kufoji muhtasari wa kikao na sahihi
za wajumbe wa kamati ya utendaji na
kupeleka benki jina la Nsia, kisha kuchota
fedha hizo zaidi ya bil 1 kwa matumizi
yao binafsi ya kampeni za chaguzi za
mikoa bila idhini ya Kamati ya Utendaji.
Ndugu zetu mliopewa dhama PCCB
chonde chonde acheni kumtazama nyani
usoni, mna vielelezo vyote kuhusu
kuchotwa kwa fedha hizo, muhtasari
uliofojiwa pamoja na sahihi za wajumbe,
ila mbona hamuwafikishi kizimbani
wahusika?
Naomba kuwasilisha.....

Comments

Popular posts from this blog

KILOMETERS KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA MIKOANI

NAMNA YA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH) KISHERIA

MAANA HALISI YA NENO KATERERO