Ishu ya madawa inaendelea

*Drug saga continues*

Gwajima responds to RC

Ikiwa kwa namna yoyote nimewahi kuona achia mbali kushika dawa za kulevya, Mungu anishushe chini.

Ikuwa Makonda anasema ili kunitia mimi kwenye shimo la moto, kama ananionea Mungu amtangulize yeye kwenye shimo hilo.

Makonda anampakazia Gwajima kuwa anahusika na biashara ya dawa za kulevya ili nani afurahi?

Makonda mwenyewe anajua kuwa mimi nimeokoka na alikuja kanisani kwangu na nikamuombea.

Makonda ajiulize, kwa kauli zake alizozitoa ni wakristo wangapi wamekufa mioyo, ni wachungaji wangapi wamefedheheshwa.

Kama mimi najihusisha na dawa za kulevya, ningekamatwa kipindi cha uongozi wa Rais Kikwete kwa jinsi nilivyomkosoa.

Mtakumbuka Makonda alishasema Waziri Mkuu ameruhusu shisha, mara amehongwa milioni 5, mara Kamanda Sirro hawezi kazi.

Kama Kamanda Sirro kweli hawezi kazi, kwanini Makonda hakumwambia ndani ya Kamati ya Ulinzi ya Mkoa ambayo yeye ni M/kiti?.

Makonda anasema mimi ni kaka yake, huo ni unafiki, huwezi kuniita kaka alafu ukanitaja kwenye jambo la picha mbaya.

Watu wengi wanadhani Makonda ametumwa na rais, na hakuna Waziri anayezungumza kwa kuogopa, lakini Makonda hajatumwa.

Mtu mwenye uwezo wa kuniambia mimi kwenda polisi si Makonda bali ni polisi, lakini polisi hawazungumzi sababu wanaogopa.

Makonda amejiweka sehemu akajiona kama yeye ni mkuu wa wakuu wa mikoa yote.

Lakini nimpongeze Makonda kwa uajsiri wake, anaweza kuwa kiongozi mzuri siku zijazo lakini kuna vitu muhimu amekosa.

Rais Magufuli humpongeza kila anayefanya vizuri, lakini haimaanishi kupongezwa na rais juzi basi ametumwa na na rais.

Hata kama sikumuunga rais mkono kwenye kampeni lakini sasa nam-'support' hawezi kuendesha nchi Baraza la Mawaziri likiwabubu.

1. Namuomba Rais Magufuli amkanye Makonda, chuki zake kwa mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye mfumo wa serikali.

2. Makonda ni kijana mwenye ujasiri na kasi, lakini kazi ya uongozi haiwezi, namuomba Rais Magufuli amtafutie kazi nyingine.

"Makonda hajapevuka kufikia kiwango cha utawala".

Kazi ya utawala inahitaji uvumilivu, uwavumilie hata wale ambao hukubaliani nao kitu ambacho Makonda hakiwezi.

Comments

Popular posts from this blog

KILOMETERS KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA MIKOANI

NAMNA YA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH) KISHERIA

MAANA HALISI YA NENO KATERERO