MANENO YA WAZIRI WA ARDHI MH. LUKUVI KUHUSU DIASPORA NA UMILIKI WA ARDHI NCHINI TANZANI
::Utanzania na uzawa ni Mungu sio siasa "Lukuvi"::
Mimi na Watanzania wengi tulioko nje tutaendelea kuwa Watanzania kihalisi hata kama tupo China, Europe, America, nchi za Africa......
Utanzania wetu hautokani na passport au nani yuko madarakani na hautabadilika kwasababu Utanzania tumepewa na Mungu na si binadamu. Kitendo cha Lukuvi kusema Watanzania tunaoishi nje na wengine kuchukua passport hawana haki ya kumiliki ARDHI inaelekea hajui vizuri kwamba hii inagusa familia, mila zetu na kutikisa nchi yetu kuliko wakati wowote Tanzania.
Je utachukua shamba langu la babu ambalo kuna makaburi kabla ya uhuru wa nchi kwasababu eti nimechukua passport ya nchi nyingine je unafikiri hata ndugu zetu wataruhusu hilo!. Unavyoserma kukana uraia je una ushaidi gani watu kukana uraia .
Hizo ni sheria tu lakini Watu wengi wanao utaka uraia wa nchi waishizo haina maana hawautaki utanzania lakini jiulize sheria za kusoma nchi hizi ili upate scholarships unahitaji uraia, bima za afya, bima za watoto...., kazi sasa mnataka Watanzania wafanye kazi za Housegirl huko nje tu!.
Tanzania kwa sasa hakuna hata kazi za kutosha tungerudi wote hapo tungesaidia vipi familia zetu jiulizeni. Mbona nchi zingine za Kenya, Uganda..... nk hawana sheria za kijinga hivi. Unaweza kuwanyima kupiga kura lakini kuwanyima ardhi ni kichekesho na watu wako tayari kufa kwasababu hii sio issue ndogo au ya kisiasa kama watu wengine hapa wanavyojaribu kuifanya.
Kesho na kesho kutwa hujui watoto wako watakuwa wapi!! hii ni issue ya Watanzania wote. Lukuvi ni lazima aelewe sababu za wenzake wa nyuma kutowaingilia Watanzania wenzetu kwa vigezo vya sheria za miaka ya 60's hata Nyerere kwa sasa angeona mazingira tofauti.
Badala ya kuangaliana Tanzania na Watanzania tunatakiwa kuangalia nchi na kujiuliza tufanye nini kuendeleza nchi yetu badala ya kuangalia kila mtu kwa uoga hata ndugu zetu wa nje. Tanzania tuna ardhi kubwa sana badala ya kuongea na majungu tukalime, na kuendeleza ardhi yetu
By Kamundu
JF-Expert Member
Source JF
Kutoka kwenye CommentsππΎ
Mkuu umeongea maneno ya maana sana hapa.
Mr Lukuvi kudhulumu haki za watu anadhani ndio Uchapaji kazi.
Sheria hio anayotumia Kutaifisha mali za watanzania ni RAIS yupi aliokuwa haijui?
Sasa iweje toka Tupate uhuru wa nchi hii MARAIS wote na WAZIRI WOTE WA ARDHI wasiwataifishe Raia wao mashamba yao na ardhi zao?
Ina maana Wale mawaziri WOOTE wa Ardhi waliotangulia Hawaipendi Nchi yao?
Hawana Uchungu na Mali Ya Tanzania?
Makosa gani waliofanya watanzania walioko nje,
Mtu amerithi Shamba la babu yake Wewe ukampokonye.?
Laana ya Wanyonge haitomuacha!
Halafu watoto wangapi wa mawaziri wenye Uraia miwili na Wana majengo mengi hapo Tanzania? Tena Makubwa makubwa na mahoteli ya kifahari.
Kama kweli Yeye anafanya anachokisema Kwanini asianze na Hao wakubwa?
Atishe wananchi njaa wanaohangaika Ughaibuni Kujikusanyia senti mbili tatu kusaidia familia zao Hapa Nchini?
Wananchi wangapi wanafaidika na Diasporas?
Wazee wangapi wanasaidiwa na vijana wao walioko Nje?
Nchi imeshindwa Kuwapatia vijana Ajira.
Leo wamekwenda nje kutafuta Rizki na Kufanikiwa Kupata Uraia wa huko, huku nyumbani anakuja Mtu anawadhulumu Haki yao.
Hii kweli Ni Haki? HUKU ndiko KUIJENGA Tanzania na watanzania?
Mtoto wa Lukuvi angekuwa ni Mmoja wa Diaspora na Yeye Lukuvi pamoja na Mkewe wangekuwa wanamtegemea huyo Mtoto akaja kununua Shamba au Nyumba akawaweka LUKUVI NA MKEWE kisha akaja waziri wa Ardhi Akawapokonya Hio Ardhi au hio Nyumba akawatupa Nje kisha Akaipiga mnada YEYE LUKUVI angeona Hio ni Sawa?
Angesema Huyo Waziri hana chuki bali Anasimamia Sheria?
Mkuu LUKUVI maisha haya sio ya milele ktk Huu Ulimwengu.
Iko siku UTAONDOKA. hio ni 100% guarantee.
Je Unaacha Legacy ipi kwa kizazi chako na Familia yako?
Wajuu wako waje kuambiwa na Wenzao kuwa Babu yako ndio chanzo cha Familia yangu kusambaratika na Kulala nje. Na wazee wangu Kufa na Maradhi ya Moyo kwa kutupwa nje na kibanda chao Kupigwa mnada.
Mungu yupo Lukuvi na nadhani hilo unalijua.
Na wewe HUWEZI kudhulumu Wanyonge na Mungu akuache eti kwa sababu kuna Sheria imekuruhusu kufanya hivyo.
Vijana wengi mmekosa ajira ya Kuwapa,
Uraia wa Nchi mbili mmewanyima,
Wanakwenda kutafuta maisha Nje huku nyumbani Mnasema Mtataifisha mashamba yao au vibanda vyao tu kwa sababu wamechukua Uraia wa Nchi Zingine. !!
Hawa Maskini za Mungu WAFANYE NINI?
Na kama wewe una Moyo wa binaadamu acha kuonea WANYONGE wanaojenga KWAO.
Hao Watanzania walioko nje HAWAKUSHINDWA kujenga KENYA au UGANDA au Kwengine Afrika . Lkn WENGI wao Wameamua KUJENGA KWAO TANZANIA.
Hii peke yake kwa Kiongozi anaependa Maendeleo Ya Nchi yake Inatosha kuwa sababu ya Ku waive sheria ya namna Hii inayoumiza wanyonge wenye Kuhangaika mchana usiku Kujenga Kwao.
Na Mwisho
je! Umeshawahi kutazama Statistics za kiasi cha pesa Diaspora wanazotuma Hapa Nchini?
Na namna Gani wanachangia ktk Uchumi wa Nchi yetu ktk Nyanja mbali mbali?
Mimi nawafahamu Diasporas wamejikusanya na kujenga HOSPITALI hapa. Ambayo inasaidia sana wananchi. Na gharama zake Nafuu.
Na wengi wamenunua Mashamba na kutoa ajira kwa ndugu zao Watanzania na kuzifaa familia nyingi za Watanzania kama wewe.
Sasa ukaichukue Hio Hospitali na hayo mashamba na hivyo vibanda Upige mnada?
Kosa lao Kujenga Nchini kwao? Au kusaidia Wananchi kadri Mungu alivyo wawezesha?
Hio ndio Haki?
Na wewe kwa moyo wote unaona Hio Ni Sawa Kabisa.?
Wakati Rais mpya wa USA Mr Trumph alipotangaza kuwa Mexicans wote wasio na Haki za kuishi America atawarudisha kwao TAIFA LA MEXICO limetanga wazi namna Wananchi wake wanapata misaada kutoka kwa watu wao walioko USA Watakavyo athirika.
Na Serikali yao imeahidi kuwasaidia hao wananchi wao wakamate wana sheria japo Kujaribu kupinga hizo Deportations.
Je WEWE MR LUKUVI hilo Umelifikiri?
Wazazi wangapi Watakosa makazi ya Kuishi au mashamba Ya kujipatia Rizki zao kama utaamua KUTAIFISHA mali ya Watoto wao wenye Uraia miwili?
ββββββββββββ
Ushauri wangu Kwako Waziri Lukuvi .
ββββββββββββ
Kama Umeamua Kuitekeleza Sheria Ktk AWAMU Hii Basi Tangaza kuwa Wale waliofanya kosa hili kwa Huruma Ya serikali hii ya Awamu ya TANO haitawadhulumu au Kutaifisha mali zao au haki zao lkn KUANZIA SASA mwenye Uraia miwili haruhusiwi Kununua Ardhi hapo.
Hili ukimshauri RAIS MAGUFULI kwa moyo wake SIDHANI KM ATALIPINGA.
Na Sidhani km Kuna Mbunge hatta mmoja atalikataa .
Na Sidhani km kuna mwananchi yyt hapa ambae ana moyo wa Kitanzania atalipinga hili.
Kwa kujua kuwa mnaowaonea Huruma Hii ni WATOTO WENU HAO HAO WA KITANZANIA walioko Nje wanatafuta Rizki tena wengi wao wako ktk MAZINGIRA MAGUMU SANA SANA.
Na Imani Utasikiliza Kilio cha mamilioni ya watanzania wenzako wanaovuja jasho Huko Nje na kuja hapa Kujenga Taifa lao walipendalo la TANZANIA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
By
kahtaan
JF-Expert Member
inasAtercru-1988 Bill Leverich https://marketplace.visualstudio.com/items?itemName=contsucepme.Descargar-Sonder--Episode-ONE-gratuita
ReplyDeletenewspromalma
Ysubgiinru Penny Brooks https://4windows.net/adobe-illustratorwith-repack-registration-key-fresh/
ReplyDeleteSoftware
download now
odadntegmye
deucicoe_po_Albuquerque Antoinette Jordan Awesome
ReplyDeleteFree download
Link
balzardfuncprev