NAMNA YA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH) KISHERIA
Anaandika Bashiri Yakubu
Kupekua( search) ni tendo ambalohufanywa na mamlaka za usalama katika maeneo mbalimbali hasa katika makazi yawatu. Mbali na makazi ya watu kupekua pia kwaweza kufanyika katika magari, treni, na vyombo vyote vya usafiri zikiwemo ndege na meli. Pia kupekua kwaweza kufanywa kwa mtu kwa maana kuwa mtu kama mtu naye anaweza kupekuliwa(search). Iwe mifukoni au wapi lakini mtu naye hupekuliwa. Kwa jina la mtaani kupekua hujulikana kwa jina la kupiga sachi. Hivyo basi kupekua na kupiga sachi ni kitu kilekile. Mbali na kuwa upekuzi waweza kufanyika sehemu nyingi kama tulivyoona makala haya yatagusa upekuzi katika maeneo ya nyumbani kwa maana kwenye makazi au maofisi. Suala la upekuzi kwa ujumla wake huongozwa na Sura ya 20, Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho 2002 na wakati mwingine Sheria ya Jeshi la Polisi Sura ya 322.1.SABABU ZA KUPEKUA.Kisheria sababu za kupekua lazima iwe ni katika kutafuta ushahidi ambao utawezesha kupatikana kwa ukweli wa jambo fulani ambalo lipo katika ngazi za upelelezi katika mamlaka fulani. Hauwezi kufanyika upekuzi nyumbani kwa mtu kwa lengo jingine na hilo likitokea basi itakuwa ni kinyume cha sheria. Sehemu inayopekuliwa ni lazima kuwepo na tetesi au uhakika wa kuwa eneo hilo upo ushahidi unaotafutwa kwa ajili kuanzisha,kuendeleza au kukamilisha upelelezi fulani. Kwa hiyo sababu kubwa ya upekuzi(search) ni kutafuta ushahidi. Hakuna upekuzi kwa ajili ya sababu binafsi.2. NANI HUTAKIWA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH).Askari polisi anayo mamlaka ya kufanya upekuzi katika nyumba yamtu. Nyumba yaweza kuwa ya makazi au ya biashara kama duka,mgahawa, hoteli, nyumba za wageni, na vyuoni na mashuleni. Zaidi maafisa wengine kama taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa au wale wa mamlaka ya chakula na dawa ( TFDA) n.k.nao wanaweza kufanya upekuzi. Isipokuwa maafisa hawa wenginekama mamlaka ya chakula na dawa wanaruhusiwa kufanya upekuzi katika yale maeneo yanayohusu ile kazi yao tu, kwa mfano dukani kukagua bidhaa basi na si kuingia mpaka chumbani kwa mtu. Hata hivyo wanashauriwa kuambatana na afisa wa polisi mara zote wanapoamua kufanya upekuzi.3. HAIRUHUSIWI KUFANYA UPEKUZI USIKU BILA KIBALI CHA MAHAKAMA.Kifungu cha 40 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kinasema kuwa hati ya upekuzi inaweza kutolewa na kutekelezwa siku yoyote na inaweza kutekelezwa kati ya muda kuchomoza au kuchwa kwa jua lakini mahakama inaweza kwa maombi ya afisa polisi au mtu mwingine yeyote ambaye imeelekezwa kwake kumruhusu kutekeleza muda wowote. Katika tafsiri ya kifungu hiki kuna mambo mawili ya msingi.Kwanza tunaona kuwa upekuzi kawaida unatakiwa ufanyike siku yoyote kati ya jua kuchomoza na jua kuchwa. Jua kuchwa ni jua kuzama. Kawaida muda wa jua kuchomoza maeneo mengi ya Tanzania ni kuanzia Sa 12 za asubuhi na ,maeneo mengine saa 11 za asubuhi. Na muda wa jua kuzama maeneo mengi ni kati ya saa 12 za jioni hadi saa moja jioni. Kwahiyo huo ndio muda wa kawaida ambao upekuzi unatakiwakufanyika kwenye nyumba za watu. Kimsingi ni muda wa mchana( day time).Pili, tafsiri inayofuata katika kifungu hicho ni pale kinaposema kuwa kwa kibali maalum cha mahakama upekuzi unaweza kufanyika muda wowote. Hapo juu tumeona upekuzi unatakiwa kufanyika katika muda maalum ambao kimsingi ni asubuhi mpakajioni (mchana). Hapa sasa tunaona kuwa upekuzi unaweza kufanyika muda wowote ikiwemo usiku wa manane lakini hii itakuwa kwa kibali maalum cha mahakama. Kwahiyo tunaona wazi kuwa ili upekuzi ufanyike usiku yapaswa kuwepo kibali cha mahakama ambacho kimeruhusu kufanya hivyo vinginevyo upekuzi wote hutakiwa kufanyika masaa ya mchana. Kwa maana hii unapogongewa usiku na askari wanaojitambulisha kuhitaji kufanyaupekuzi kwako basi kabla ya kuruhusu zoezi hilo kufanyika omba kuona kibali cha mahakamahata kupitia dirishani kwanza. ACHA KUNYANYASWA, CHUKUA HATUA.
Shukran Kwa elimu nzuri nimepata funzo
ReplyDeleteocitprespe-Billings Mary Sanchez download
ReplyDeletelandlasider