YALIYOMO KATIKA SHERIA YA MTOTO



         Yaliyomo Kwenye SHERIA ya MTOTO Na 21 ya mwaka 2009Sheria hii imegawanyika katika sehemu kuu 13 kama ifuatavyo.Sehemu ya Kwanza;Ina maelezo ya utangulizi yanayojumuisha jina la sheria na tarehe ya kuanza kutekelezwa pamoja na ufafanuzi wa maneno yaliyotumika.Sehemu ya Pili;Inatoa tafsili ya mtoto na maelezo ya jumla ya haki ya mtotoSehemu ya Tatu;Inajumuisha uangalizi na ulinzi wa watoto walio katika mazingira hatarishi. 

          Sheria hii inafafanua mazingira mbalimbali ambayo ni hatarishi kwa mtoto kama vile uyatima, kutelekezwa, kuteswa, kuzurura,kukinzana na sheria.Sehemu ya Nne;Ina maelezo yanayohusu uangalizi wa mtoto kwa njia ya malezi ya kambo. Pia sehemu hii inaainisha na kumpa majukumu mtu aliyepewa dhamana ya uangalizi wa mtoto.Aidha, inatoa masharti ya mlezi na kuwa ni kosa kumuondoa mtoto bila ruhusa kwa mtu ambaye amepewa jukumu la uangalizi wa mtoto.Pia katika eneo hili inazuia utangazaji wa taarifa au picha zinazomhusu mtoto bila ruhusa ya Mahakama.Sehemu ya Tano;Sheria katika eneo hili imeonyesha vifungu vinavyohusu malezi, ulinzi na wajibu wa wazazi kwamatunzo ya mtoto,matibabu na elimu.Pia katika eneo hili utaratibu na vigezo vya maombi ya kuwa mzazi na uthibitisho wa kuwa mzazi. 
          Maombi ya uangalizi pamoja na maombi ya utaratibu wa matunzo pia yanaainishwa hapa.Sehemu ya Sita;Ina ainisha sifa za mtu kuwa mlezi na uasili wa mtoto,utaratibuwa kuomba uasili wa mtoto, pamojana haki za mtoto aliyeasiliwa. Pia inatoa jukumu la utunzaji wa rejista ya watoto walioasiliwa kwa Msajili wa Vizazi na Vifo.Aidha, inaainisha sababu ya kuzuia au kutoa kibali kwa mtu anayetaka kumuasili mtoto na haki ya mtoto kurithi pale itakapotokea muasili amefariki bila kuweka wosiaSehemu ya Saba;Inaweka utaratibu wa kutoa ajira nyepesi kwa watoto walio chini ya miaka 14 na uzuiaji wa kazi zaudhalilishaji kwa watoto chini ya miaka 18.
          Aidha, inatoa maelezo ya jinsi mtoto atakavyochukuliwa kwa ajili ya kupewa mafunzo yakazi (apprenticeship) chini ya uangalizi wa mtu anayemfundisha baada ya kuingia mkataba maalum.Sehemu ya Nane;Inaweka wajibu kwa Serikali za Mitaa kuboresha ustawi wa mtoto katika mamlaka za Serikali ya Mtaa husika. Sehemu hii inatoa masharti na kuwekautaratibu/wajibu wa Serikali ya Mtaa kuingia mahalipopote kwa ajili ya kutoa msaada pale ambapo itaonekana haki za mtoto zinakiukwa.Aidha, Mamlaka ina uwezo wa kushirikiana na Polisina Afisa wa Ustawi wa Jamii, kuchunguza au kutafuta mtoto aliyetelekezwa kupotea au kufichwaSehemu ya Tisa;Inapendekeza kuundwa kwa Mahakama Maalum yaWatoto ambayo itashughulikia masuala yanayohusuwatoto . Pia Sehemu hii inaweka taratibu za uendeshaji wa shauri kwenye Mahakama ya Watoto.Sehemu ya Kumi;Inaweka masharti kuhusu uanzishaji na uendeshaji wa shule maalum za watoto.
          Sehemu ya Kumi na Moja;Inaweka masharti ya uanzishwaji wa vituo vya kutunzia na kulelea watoto wenye shida ya malezi, kusimamia na kuendesha vituo hivyo pamoja na utaratibu wa kuwapokea watoto.Aidha, sehemu hii inaainisha majukumu ya mameneja, wasimamizi na wafanyakazi wa vituo hivyo.Sehemu ya Kumi na Mbili;Inaweka masharti ya jumla ambayo yana ainisha mamlaka ya Waziri mwenye dhamana ya watoto kutunga kanuni na Taratibu za Sheria.Sehemu ya Kumi na Tatu;Inahusu kufutwa baadhi ya Sheria pamoja na kufanya marekebisho kwenye baadhi ya Sheria ambazo zinagusa masuala ya watoto ili masharti yaSheria hizo yaoane na masharti ya Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009.

HITIMISHO
          Sheria ya Mtoto, 2009 imeshaanza kutekelezwa- Jamii kwa mujibu wa Sheria hii inawajibu wa kuzingatia na kuifuta.- Kushindwa kutekeleza wajibu huo kutasababisha kuchukuliwa hatua za kisheria.- Tuisome na kuielewa Sheria hii kwa manufaa ya utekelezaji wa Haki na Ustawi wa mtoto wa Tanzania.---Mathias Haule, Afisa maendeleo ya jamii masuala ya ukatili dhidi ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akielezea kwa kifupi kuhusu Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka2009.Hii ni sehemu tu ya mafunzo ambayo watangazaji na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto wanaendelea kuyapata katika Warsha kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhdi ya Watoto inayofanyika mjini Moshi.

Comments

Popular posts from this blog

KILOMETERS KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA MIKOANI

NAMNA YA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH) KISHERIA

MAANA HALISI YA NENO KATERERO