SHERIA YA JINAI TANZANIA BARA KUPITIA KANUNI YA ADHABU (PENAL CODE)
SHERIA YA JINAI TANZANIA
Sheria ya jinai Inahusika na makosa ambayo yanapotendeka mtu anayehusika na utendaji wa makosa hayo anaweza akakamatwa,kushitakiwa na kupewa adhabu na mahakama ya sheria, sheria hii inahusika na ulinzi wa haki kwa matakwa ya serikali, makosa mengi ya jinai yako chini ya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kwa Tanzania bara na kanuni ya adhabu ya Zanzibar sura ya 13.
UHALIFU:-maana ya uhalifu ni tabia au kutenda kitendo chochote ambacho sheria imekataza kufanyika kwa kitendo hicho na kwa upande mwingine MHALIFU ni mtu yeyote yule anayetenda vitendo au kitendo ambacho kimekatazwa na sheria zilizowekwa.
Makosa ya jinai ni kutenda kitendo au kujaribu kutenda kitendo au kuacha kutenda kitendo ambacho kinakatazwa na kinaadhibika na sheria zilizowekwa.
Hatua mbalimbali za ufanyikaji wa kosa la jinai au Kwa maana nyingine ili kosa la jinai liwe limefanyika kuna hatua lazima liwe limepitia, hatua hizi au vigezo vya ufanyikaji wa kosa la jinai ni vigezo muhimu Sana ambavyo huangaliwa na mahakama zote endapo kosa litafanyika na kesi kupelekwa mbele ya Mahayana.
Vigezo hivi viwili vya utendaji wa kosa ni (1). Actus reus (tendo ovu lenyewe) pamoja na (2). Mens rea (nia ovu )
NIA OVU (MENS REA)Nia ovu ni mawazo potofu au nia mbaya ambayo mtu anakuwa NATO kwa lengo la kutenda kosa ,vile vile nia hii ovu imegawanyika katika vipengele mbalimbali kama ifuatavyo:-
(i) INTENTION (NIA) maana yake ni pale Hali ya mawazo ya mtu ambayo atakuwa anajua athari ya kitendo au tabia yake lakini pia anataka matokeo ya kitendo chake yawe hivyo Kama Alivyonuia, Mfano iwapo mtu atamlenga mtu mwingine na bunduki iliyo na risasi ndani yake, kisha akamfyatulia risasi na kumuua, mtu huyo si tu kwamba alifahamu matokeo ya kitendo chake lakini pia alinuia madhara ya kitendo hicho.
(ii) RECKLESSNESS (KUTOKUJALI) hii ni hali ya mtu ambayo anatenda kitendo kwa kukaribisha matokeo yake lakini bila ya kujali anaendelea kutenda kitendo hicho, mfano dereva akiendesha gari kwenye mtaa wenye watu wengi kwa mwendo Wa kasi wakati akijua wazi kwamba anaweza kusababisha ajali, lakini bila ya kujali matokeo au madhara yake kwa kupunguza mwendo anaendelea kuendesha kwa mwendo wa kasi na kugonga may. Kwa hali hii ndio tunasema kwamba mtu huyu ni reckless.
(iii) NEGLIGENCE (KUZEMBEA) ni hali ya mawazo ya mtu ambaye anatenda kitendo au anaacha kutenda kitendo ambacho Kama mtu mwingine mwenye busara na akili timamu alipaswa kujua matokeo ya kitendo chake na kukizuia. Mfano ni mlinzi anapaswa kufunga mlango mkuu wa kiwanda fulani lakini bila sababu siku moja hakufunga mlango huo na matokeo yake wezi waliingia ndani ya kiwanda na kuiba mali iliyokuwa imehifadhiwa eneo la kiwanda hicho.
Tendo ovu ni kitendo cha wazi ambacho ni matokeo ya utekelezaji wa nia ovu iliyoundwa hapo awali.
TOFAUTI KATI YA SHERIA JINAI NA MADAI
1. Sheria ya jinai inahusika na uhalifu kwajili ya ya haki ya umma kwa ujumla wakati sheria ya madai inahusika na mashauri ya binafsi ambayo ni kwajili ya kulinda haki za mtu bonsai.
2. Sheria ya jinai lengo lake ni kuzuia makosa nakuwaadabisha watu ambao ni wahalifu wakati sheria ya madai madhumuni ni kuwasaidia watu binafsi kupata haki zao wanazodai, humwezesha mtu kudai fidia kutoka kwa mtu mwingine kutokana na madhara na kashfa aliyomfanyia..
3. Sheria ya jinai huhitaji chombo cha kiserkali katika kufanya upelelezi, mfano Police ili kuweza kutambua, kuwakamata na kuwashitaki wahalifu, lakini kwa upande wa sheria ya madai huwa haihusishi chombo chochote cha dola kuifanyia upelelezi, mtu mwenyewe anayekosewa ndio hufanya uchunguzi.
KUTOKUJUA SHERIA kifungu 8 kanuni ya adhabu ambapo kifungu hiki kinaeleza ya kwamba kutokujua sheria hakutamfanya mtu kupata msamaha kutokana na au kuacha kutenda, japokuwa kunaweza kuwa utetezi wakati tu sheria yenyewe itakuwa imetamka wazi kuwa ufahamu wa sheria hiyo ni moja ya kigezo kinachounda kosa linalohusika.
DAI LA HAKI kifungu namba 9cha sheria ya kanuni ya adhabu kinatamka ya kuwa mtu hatakuwa na jukumu la jinai kwa kosa atakalotenda linalohusiana na Mali Mali ikiwa kitendo kitendo kilichotendwa alikifanya akiwa na dai la haki na alifanya alifanya dai hilo kwa njia uamunifu na bila ya kuwa na nia ya kudanganya au kudhulumu, hivyo ili mtu apate utetezi chini ya kifungu chini ya kifungu hiki ni lazima vigezo vifuatavyo vithibitishwe (a) dai hilo lihusiane na Mali, (b) dai hilo lifanywe kwa njia ya uaminifu (c) kusiwepo na nia ya kudhulumu au kudanganya.
KUKUSUDIA NA SABABU kifungu namba 10 cha kanuni ya adhabu ambapo kinatamka ya kuwa kuhusiana na vitendo vya uzembe mtu hatakuwa na jukumu la jinai kutokana na kitendo ambacho kitatokea bila ya yeye kukinuia au tukio ambalo litatokea kwa bahati mbaya au kwa ajali.
KUKOSA UHAKIKA kifungu namba 11 cha sheria ya kanuni ya adhabu,mtu hatakuwa na jukumu la jinai ikiwa atatenda kitendo au kuacha kutenda kitendo iwapo kufanya hivyo kwa uaminifu na busara katika Hali ambayo aliamini kwamba hali ya mambo ingelikuwa Kama alivyodhamiria au kutarajia.
Comments
Post a Comment