UNALOPASWA KULIJUA LEO: MAJUKUMU YA MAMLAKA MBALIMBALI ZA KISERIKALI BARABARANI. 1. SUMATRA: Anahusika na kusimamia mwenendo wa sekta ya usafirishaji. Yaani sekta hiyo iwe na utaratibu, isiwe na vurugu, na wachezaji ambao ni wasafirishaji wacheze kwa kufuata fair play kwa faida ya walaji ambao ni abiria. Kwa hiyo SUMATRA ni kama refa. Ndio maana anaitwa mdhibiti. Yeye anadhibiti watoia huduma na pia kuwawekea mazingira bora ya ushindani na kibiashara.Hawa sheria yao kuu ni SUMATRA ACT, TRANSPORT LICENSING ACT na kanuni zake.Chini ya sheria hizo wanatunga kanuni mbalimbali. ASICHOHUSIKA NACHO: Hahusiki na miundombinu ya barabara, wala ajira za madereva, wala alama za barabarani. SUMATRA ipo chini ya wizara ya uchukuzi. 2. TANROADS: Huyu yeye ni wakala wa miundombinu ya barabara. Yeye ndiye anahusika na ujenzi wa barabara, viwango vya barabara, madaraja, upana wa njia, alama za barabarani, na mizani. Hawa sheria yao kuu ni THE ROADS ACT 2007, na kanuni zake na kanuni zilizo chin...