HII NDIYO MAANA HALISI YA NENO KATERERO Rafiki yangu mpendwa, naandika maneno haya nikiwa na uhakika kuwa yatakufikia na kuweza kukutoa katika kifungo cha mawazo. Ni wajibu wangu na ni haki yako pia, mimi kuweza kujitahidi kwa vyovyote vile niwevyo ili niweze kukutoa katika kifungo hicho. Kuendelea kukuacha katika hicho kifungo eti kisa mimi sijafungwa kimwili, nitakuwa najidanganya kwani kama sijafungwa kimwili, nitafungwa kiroho. Ninaweza kukosa hata nafasi ya kuuonja utamu wa milele kwani nitakuwa na kesi ya kujibu huko mbeleni kwa maana Muweza Wa Yote anasema kuwa , “ Amuachaye mwenzie akaangamia ilihali anao uwezo wa kumnusuru atakuwa amejiangamiza yeye mwenyewe”. Kwa mantiki hiyo sasa, nataka nikunusuru wewe usiangamie pamoja na mimi pia kwa kukutoa katika kifungo cha maana ya neno KATERERO. Ikumbukwe kuwa ni wazi na ukweli usiopingika kuwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na upindishaji wa lazima wa maana ya neno KATERERO. Watu wengi tena wenye akili zao, ambao wangekuwa...
Comments
Post a Comment