HARAKATI ZA HAKI ZA BINADAMI NA MAHAKAMA ZA TANZANIA

From Yona Fares

JAJI MWALUSANYA VS HUKUMU YA KIFO.

Mwaka 1994 katika mahakama kuu mkoani Dodoma mbele ya Jaji Mwalusanya J, watu wawili Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula walikutwa na hatia ya kosa la mauaji ambapo waliua mtu na kupora mifugo yake. Walikutwa na kosa la mauaji ya kukusudia (murder) kinyume na kifungu cha 196 cha Penal Code Cap 16. 
Walitakiwa kupewa hukumu ya kifo kwa mujibu wa kifungu cha 197 cha Penal Code, Kunyongwa mpaka kufa kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Penal Code.

Kabla jaji hajatoa hukumu wakili wa Mbushuu na Sungula wakili Rweyongeza aliibua hoja kuhusiana na adhabu ya kifo kwamba hukumu ya kifo ni kinyume kabisa cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 ibara 13(6)(d) na (e) kwa maana kwamba hukumu ya kifo ni ya kikatili,ya mateso, inayotweza utu wa mtu na isiyo ya kibinadamu. Wakili Rweyongeza alienda mbali zaidi na kusema hukumu ya kifo ni kinyume cha katiba ibara ya 14 inayotoa haki ya kuishi, kwa hoja hizo aliiomba mahakama isitoe hukumu ya kifo kwa wateja wake kwani hukumu hiyo ni unconstitutional!

Jaji Mwalusanya alikubaliana moja kwa moja na wakili Rweyongeza kwanza kwamba hukumu ya kifo ni adhabu ya mateso, kinyume cha utu na ubinadamu na ya kikatili, Jaji Mwalusanya alisema ukatili wa hukumu ya kifo unaonekana katika utekelezaji wa hukumu wake kwani si wa kistaarabu hata kidogo.

"One leading doctor described the process as slow, dirty, horrible, brutal, uncivilized and unspeakably barbaric"
Mwalusanya anasema mfungwa huachiwa umbali wa 8 feet akiwa amefungwa kitanzi shingoni lengo likiwa ni kuvunja shingo yake ili afe haraka na mara nyingine iwapo mnyongaji amemkosa mfungwa kisawasawa au shingo haijavunjika ipasavyo basi mnyongaji humpiga mfungwa risasi ya mguu au humpiga na nyundo kichwani kuharakisha kifo chake.

Mwalusanya anasema serikali inawafundisha raia kuua kwa kutekeleza hukumu ya kifo. Kama serikali inataka raia waheshimu maisha ya watu basi serikali inatakiwa iache kuua. Kama kila anayeua ni lazima naye auawe kwanini serikali isiajili wabakaji maalumu kwa ajili ya kuwabaka wale wanaobaka wengine badala yake hukumu ya ubakaji ni miaka 30 jela. Kuthibitisha kuwa hukumu ya kifo ni ya kikatili kinyume cha utu serikali inakumbwa na guilt conscience yaani inasutwa na ndiyo maana hata hukumu ya kifo hutekelezwa kwa usiri mkubwa mno.

Jaji mwalisanya anasema hukumu ya kifo ni kinyume na ibara ya 14 ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayotoa haki ya kuishi kwa kila mtanzania. Sababu zingine ni ucheleweshwaji wa utekelezaji wa hukumu hiyo ya kifo na mazingira mabaya ambayo wafungwa wanaosubiri kunyongwa huhifadhiwa.

Jaji Mwalusanya baada ya kupinga vikali kicriticise vikali kifungu cha sheria cha kanuni ya adhabu ya makosa ya jinai (Penal Code) kifungu cha 197 na kukitangaza kuwa kinapingana na katiba yaani Unconstitutional, aliwahukumu Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula kifungo cha maisha jela kila mmoja badala ya hukumu ya kifo.

Cha ajabu Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula walikata rufaa kwenda mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sababu kwamba hawakuridhishwa na ushahidi uliotolewa dhidi yao na kwamba hawakuhusika na mauaji yoyote.

Katika mahakama ya Rufani ya Tanzania Corum ya majaji watatu ambao ni Lubuva J, Ramadhani J, na Makame J ilipokaa na kusikiliza rufaa hiyo. Majaji wa mahakama ya Rufani walijikita kwenye kuipinga vikali hukumu ya Jaji Mwalusanya, kwanza walikubaliana rufaa kwamba ushahidi hautoshelezi, pili walitengua hukumu iliyotolewa na Jaji Mwalusanya ya kifungo cha maisha kwa watuhumiwa hao badala yake waliwaachia huru Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula. Pamoja na hayo walipinga vikali hoja za Mwalusanya dhidi ya hukumu ya kifo
Katika hoja zao majaji wa Rufani huku wanasema Mwalusanya alikosea kutangaza kifungu cha 197 cha Penal Code kuwa unconstitutional kwani haki ya kuishi inayotolewa kwenye katiba ibara ya 14 siyo absolute inatakiwa kuwa subjected to the law, kwa maana kwamba kila mtu ana haki ya kuishi kwa mujibu wa sheria hivyo kama ukivunja sheria haki yako ya kuishi inaondolewa kwa mfano sheria imekataza kuua hivyo ukiua haki yako ya kuishi inaondolewa kwa wewe pia kuhukumiwa kifo. Sababu ya pili ni ibara 30(2) ya katiba inayoruhusu kutotekeleza baadhi ya haki kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa mahakama ya Rufani hukumu ya kifo hutolewa kwa maslahi ya umma ili kuilinda jamii dhibi ya wauaji, kwamba jamii haipendi watu waue hivyo kuweka hukumu ya kifo ni kuilinda jamii dhidi ya mauaji.

Kwa hukumu hii ya mahakama ya Rufani ya Tanzania hukumu ya kifo inaendelea kuwa halali nchini Tanzania japokuwa in practical hukumu hii imekuwa haitekelezwi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 18 sasa hali ambayo imepelekea walio hukumiwa kifo kufikia zaidi ya mia nne gerezani nchini Tanzania. Hii inatokana na kelele nyingi sana kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu na jumuiya za kimataifa.

Comments

Popular posts from this blog

KILOMETERS KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA MIKOANI

NAMNA YA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH) KISHERIA

MAANA HALISI YA NENO KATERERO