UNALOPASWA KULIJUA LEO: MAJUKUMU YA MAMLAKA MBALIMBALI ZA KISERIKALI

UNALOPASWA KULIJUA LEO:
MAJUKUMU YA MAMLAKA MBALIMBALI ZA KISERIKALI BARABARANI.
1. SUMATRA:
Anahusika na kusimamia mwenendo wa sekta ya usafirishaji. Yaani sekta hiyo iwe na utaratibu, isiwe na vurugu, na wachezaji ambao ni wasafirishaji wacheze kwa kufuata fair play kwa faida ya walaji ambao ni abiria. Kwa hiyo SUMATRA ni kama refa. Ndio maana anaitwa mdhibiti. Yeye anadhibiti watoia huduma na pia kuwawekea mazingira bora ya ushindani na kibiashara.Hawa sheria yao kuu ni SUMATRA ACT, TRANSPORT LICENSING ACT na kanuni zake.Chini ya sheria hizo wanatunga kanuni mbalimbali.
ASICHOHUSIKA NACHO:
Hahusiki na miundombinu ya barabara, wala ajira za madereva, wala alama za barabarani.
SUMATRA ipo chini ya wizara ya uchukuzi.

2. TANROADS:
Huyu yeye ni wakala wa miundombinu ya barabara. Yeye ndiye anahusika na ujenzi wa barabara, viwango vya barabara, madaraja, upana wa njia, alama za barabarani, na mizani. Hawa sheria yao kuu ni THE ROADS ACT 2007, na kanuni zake na kanuni zilizo chini ya ROAD traffic Act kuhusu uzito na urefu wa magari. Hawa hawahusiki kabisa na ajira ya dereva, wala utoaji wa leseni au upangaji wa timetable.Chini ya sheria hizo wanatunga kanuni mbalimbali.
TANROADS ipo chini ya wizara ya Ujenzi.

3. TRAFIKI POLISI.
Hawa wanahusika na kulinda usalama wa raia na mali awapo barabarani. Na wao wanasimamia utekelezaji wa sheria karibu zote zinazohusu barabara. ziwe za TANROADS,sumatra au za usalama barabarani. Wao sheria yao kuu inaitwa THE ROAD TRAFFIC ACT cap 168, na kanuni zake.Chini ya sheria hizo wanatunga kanuni mbalimbali.
Hawa hawahusiki kabisa na miundombinu ya barabara au ajira za madereva. ila wanahusika kulinda miundombinu isiharibiwe.
TRAFIKI POLISI wapo chini ya wizara ya mambo ya ndani.

4. HALMASHAURI ZA MJI NA MAJIJI.
Hawa wanahusika na miundombinu ya barabara zilizochini ya mikoa na halmashauri. stendi zote zipo chini yao na hutunga kanuni za matumizi bora ya stendi pamoja na taa za barabarani za maeneo waliyopo. Sheria yao kuu ni LOCAL GOVERNMENT(DISTRICT AUTHORITIES) ACT, 1984 na ile ya LOCAL GOVERNMENT (Urban authorities) Act 1984 na sheria nyingine nyingine za masuala ya fedha. Chini ya sheria hizo wanatunga kanuni mbalimbali.
Halmashauri zipo chini ya Wizara ya Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

5. KAMISHANA WA KAZI.
Wizara hii ndio hushughulia masuala yote ya ajira nchini Tanzania. Kazi yao ni kuhakikisha kunakuwa na soko la ajira linalofuata sheria na kanuni. wafanyakazi wanakuwa na mikataba, na pia kuweka viwango vya mishahara na masharti mbalimbali ya ajira. Hawa wanatekeleza sheria ya kazi. EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT, LABOUR INSTITUTIONS ACT na sera za kazi.
Kamishna wa kazi na maafisa wake wa kazi wapo chini ya WIZARA YA KAZI, AJIRA WAZEE NA WALEMAVU.
Wizara hii pia hushughulikia utatuzi wa migogoro ya kazi kati ya mwajiri na mwajiriwa chini ya chombo kiitwacho CMA-COMMISION FOR MEDIATION AND ARBITRATION. Migogoro ya kazi huanzia kwenye chombo hiki hadi kufika MAHAKAMA YA KAZI.

6. TBS
Hili ni shirika la viwango. Kazi yake kubwa ni kuweka viwango vya mambo mbalimbali nchini Tanzania. barabarani wanahusika zaidi na viwnago vya mabasi, tairi, mabodi, helmeti, barabara, nk.

Kwa hiyo utaona kuwa kila chombo hapo kina kazi yake na sheria zake na msimamizi wake. Huwezi kutaka sumatra watunge sheria kuhusu alama za barabarani haiwezekani. Hapo inakuwa sawa na kusubiri NAZI chini ya mwembe.
UKIJUA KAZI YA KILA MAMLAKA HAPO HUWEZI KUCHANGANYA MAMBO.
Naamini kwa post hii umepata kuelimika kidogo, na itakusaidia usichanganye madesa.
RSA TANZANIA.
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.

Comments

Popular posts from this blog

KILOMETERS KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA MIKOANI

NAMNA YA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH) KISHERIA

MAANA HALISI YA NENO KATERERO