TAMBUA HAYA NDIYO MAKOSA YANAFANYIKA WAKATI WANANDOA WANAPOKWENDA KULALA
Wapenzi wengi wanaishi kwa mazoea, hawajui nini wafanye na nini wasifanye kwa ajili ya kupalilia mapenzi yao na matokeo yake, inakuwa rahisi mume kumchoka mke au mke kumchoka mume kwa sababu ya vitu ambavyo wahusika wenyewe ndiyo wamevikaribisha. Yapo makosa ambayo watu wengi wamekuwa wakiyafanya wawapo chumbani na wenzi wao, iwe ni kwa kujua au kwa kutokujua. Hakuna muda wa muhimu kwa wanandoa au wapenzi wanaoishi pamoja, kama ule muda kabla hamjapitiwa na usingizi. Ukiwa makini, utayafurahia mapenzi lakini ukikosa umakini na kuyafanya makosa yafuatayo, utakuwa unaiua ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe. Yafuatayo ni makosa ambayo wapenzi wengi huyafanya kila siku na kusababisha mapenzi yapungue taratibu: KWENDA KULALA MUDA TOFAUTI Yawezekana watu wengi wanalichukulia suala la kila mmoja kwenda kulala kwa wakati wake kama jambo la kawaida. Kwamba wanandoa au wapenzi wanaishi pamoja lakini kila mtu ana ratiba yake ya kwenda kulala, huyu akiwahi leo kupanda kitandani, yule anachelew...